JAJI KIONGOZI AZUNGUMZA NA WATALAAMU KUTOKA BENKI YA DUNIA KUHUSU MABORESHO YA MAHAKAMA | ZamotoHabari.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Eliezer Feleshi(wa pili kulia) akizungumza kuhusu mafanikio ya Mradi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano (2015/2016 mpaka 2019/2020) kwa ujumbe kutoka Benki ya Dunia( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma. (watatu kushoto) Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Benis Biseko (wanne kushoto) ni Msaidizi wa Mtendaji wa Mkuu wa Tanzania,Ginaweda Nashon.Kulia wa kwanza (kushoto) ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Deborah Isser, wa pili kushoto ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Waleed Malik na watatu (kushoto) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha.
Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (JDU)Mhe. Zahara Maruma (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Wataalamu wa Benki ya Dunia, (wa pili) ni Deborah Isser, (wa pili kushoto) ni Waleed Malik na wa kwanza ni Denis Biseko.
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia,Deborah Isser(wa kwanza kulia ) akifafanua jambo kuhusu ueneshaji wa kesi kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’,(wa pili kulia) ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Waleed Malik na (watatu ni kulia) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha.

***************

Na Aziza Muhali (SJMC)

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt, Eliezer Feleshi, amefanya mazungumzo na wadau kutoka Benki ya Dunia(WB) juu ya tathmini ya Mradi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania yanayofanywa chini, ambapo umeleta matokeo chanya katika shughuli za Mahakama.

Akizungumza na ujumbe wa benki hiyo, katika ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi alisema mradi huo, umeweza kusaidia kuboresha shughuli za utendaji kazi wa Mahakama na kusogeza huduma karibu na wananchi.

“Tumeweza kusikiliza kesi kwa kutumia Mahakama Inayotembea (Mobile Court) jijini Mwanza, hivyo ni moja ya maboresho ya huduma za Mahakama, yaliyotokana na mradi huu,” alisema Jaji Kiongozi.

Aliongeza kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki hiyo, umewezesha Mahakama ya Tanzania,kusikiliza kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video coference’, ambapo, ugeni huo, ulitaka kufahamu tathimini ya eneo hilo, alisema umeweza kutumika katika baadhi ya mikoa,ambayo ni Mbeya, Bukoba, na Kituo cha Mafunzo cha kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyo-Dar es Saalam, kikiwemo Chuo cha Uongozi wa Mahakama(IJA) Lushoto.

Jaji Kiongozi amefafanua mkakati wa kupata ukumbi(chumba maalum) kwa ajili ya kuanzisha kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao katika gereza la Keko Jijini Dar es Salaam.

Jaji kiongozi amefafanua changamoto zinazoikabili Mahakama ikiwa ni pamoja na upungufu wa kumbi maalumu za kuendeshea kesi kwa njia hiyo,‘Tunakabiliwa na upungufu wa kumbi maalumu kwa ajili ya kuendeshea kesi, hivyo tunatakiwa tupate kumbi nyingi ili tuweze kuendesha kesi kwa wakati.

Aliongeza kwamba kwa hivi sasa ni ukumbi mmoja ndio unaotumika kuendesha kesi kwa njia hiyo’, alisema Mh. Dkt. Jaji Kiongozi.Aliyataja mafaniko mengine ni Mfumo wa Kusajili kesi kwa njia ya Kielektroniki(JSDS).

Dkt. Feleshi alisema eneo lingine, ambalo litafanyikazi ni kuhusu ambayo upelelezi wa kesi kuchukua muda mrefu ambapo kesi moja inaweza kuchukua kati ya mwaka mmoja au zaidi, hivyo litawekewa muda maalum.

Wadau hao , waliwasili nchini mnamo Agosti 23 mwaka huu , watakuwepo nchini hadi Agosti 31, mwaka huu, wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama ikiwemo Mahakama ya Kuu ya Musoma, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu na kufanya ziara Mkoani Dodoma na Mwanza ambako walijionea hali halisi ya utendaji kazi wa Mahakama Inayotembea.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini