Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Ndulu katika mkutano wahadhara uliofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge Kingu akikagua ujenzi wa nyumba ya Walimu katika Shule ya Msingi Ndulu ambapo pia alikagua Zahanati ya kijiji hicho.
Mbunge Kingu akikagua ujenzi wa matundu ya choo ya Shule ya Msingi Ndulu.
Burudani zikiendelea zikiongozwa na Msanii Monko Monko.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndulu, Joseph Mwanga akizungumza kwenye mkutano huo.
Viongozi wa Kata hiyo wakijitambulisha.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Juma Ntandu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akikaribishwa kuhutubia kwa burudani za nyimbo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema Serikali inatarajia kujenga barabara ya kiwango cha changarawe kutoka Kata ya Ihanja iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida hadi Kijiji cha Ndulu yenye urefu wa zaidi ya kilomita 15.
Hatua hiyo imefikiwa kutokana na kilio cha muda mrefu cha wananchi wa kijiji hicho kutokuwa na barabara ya uhakika hivyo kuwa na changamogo kubwa hasa wakati wa mvua za masika.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara Kingu alisema tayari Serikali imepitisha zaidi ya sh.milioni 287 za ujenzi wa barabara hiyo kinachofanyika hivi sasa ni kufanya usanifu na kumpata mkandarasi atakayeanza kazi hiyo haraka iwezekanavyo.
"Kazi hiyo itakapoanza vijana mkae mkao wa kula kwani mtapata ajira hivyo atakayehitaji kufanyakazi awe tayari kwani ni fursa hiyo kwenu" alisema Kingu.Katika hatua nyingine Kingu alisema Serikali imetoa sh.milioni 170 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabwalo ya wanafunzi wa Sekondari katika kata hiyo ya Ihanja.
Mbali ya miradi hiyo Kingu alisema wananchi wa kijiji hicho wakaetayari kupata Umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao utatoka makao makuu ya Kata ya Ihanja hadi katika kijiji hicho ambapo pia aliahidi kuwapelekea jokofu la kutunzia dawa za chanjo katika Zahanati yao ili kuwapunguzia safari ndefu ya kwenda kupata dawa hizo Kituo cha Afya cha Ihanja.
" Nimesikia kilio chenu cha kutokuwa na jokofu nitakwenda Bohari ya Dawa (MSD) kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu Laurian Bwanakunu ili nione atatusaidiaje kupata jokofu hilo" alisema Kingu.
Kingu alisema miradi yote hiyo inafafanywa na Serikali baada ya Rais Dkt.John Magufuli kubana mianya ya wizi wa fedha za selikali ambazo zilikuwa zikitumika vibaya na kuzielekeza kufanya miradi ya maendeleo ya wananchi.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments