Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Watumishi wa wizara ya Katiba na Sheria baada ya kuwasili katika Banda la Wizara katika Viwanja vya Nyakabindi kwenye maonyesho ya kitaifa ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika wilayani Batiadi mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akisalimiana na Wasajili Wasaidizi Msaada wa sheria kutoka katika wilaya za Mkoa wa Simiyu wanaoshiriki maonyesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa mkoani Simiyu
Mhe. Mtaka akizungumza na Wasajili Wasaidizi waliopo kulia alipotembelea Banda la Wizara ya Katiba na Sheria mjini Bariadi katika maonyesho ya kitaifa ya Wakulima maarufu Kama Nane Nane
Mhe. Mtaka akizungumza na Wasajili Wasaidizi waliopo kulia alipotembelea Banda la Wizara ya Katiba na Sheria mjini Bariadi katika maonyesho ya kitaifa ya Wakulima maarufu Kama Nane Nane
Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria bi Agness Tumbuchile akifafanua Jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alipotembelea Banda la Wizara katika Viwanja vya Nyakabindi mjini Bariadi mkoani Simiyu ambako yanafanyika maonyesho ya kitaifa ya wakulima
Mhe.Mtaka alisisitiza kitu kwa Wasajili Wasaidizi Msaada wa sheria wa Mkoa wa Simiyu alipotembelea Banda la Wizara katika maonyesho ya wakulima Nane Name mjini Bariadi
………………………
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka wasajili wasaidizi Msaada wa Sheria mkoani Simiyu kuwasaidia viongozi wa mkoa huo katika kutatua matataizo ya wananchi kwa kuwa wao wako na wananchi hao katika kazi zao za kila siku na kuwafikisha viongozi taarifa za utatuzi wa kero hizo.
Mhe. Mtaka ametoa rai hiyo alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu ambako yanafanyika maonyesho ya wakulima Nane Nane kitaifa.
Mhe. Mtaka alikuwa akiongea bandani hapo na wasajili wasaidizi hao ambao ni maafisa maendeleo ya jamii kutoka katika wilaya za Bariadi, Meatu ,Itilima, Busega na Maswa.
“Nimefurahi kuwakuta wote hapa, niwatake mfanye kazi hii ya Msajili Msaidizi kwa nguvu zote ili muisaidie serikali kutekeleza azma yake ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi na hivyo kupata haki zao, muwasaidie viongozi kutatua matatizo ya wananchi kwa sababu sisi wanasiasa leo tupo kesho hatupo lakini nyie mpo na mnayajua matatizo ya wananchi kwani ni sehemu ya kazi zenu za kila siku, Serikali ilipoamua nyiyi mfanye kazi hii ilikuwa inajua ina maana gani“ amesema mhe. Mtaka.
Amesema ataitisha kikao cha pamoja cha wasajili wasaidizi hao na viongozi wa mkoa na wilaya zote ili kuwasikiliza wasajili wasaidizi hao juu ya historia na mwenendo wa matatizo yanayowakabili wananchi kutoka katika maeneo yao na namna wanavyoyatatua ili kuwawezesha wananchi kupata utatuzi wa kudumu na sio kila siku wanapokuja viongozi wapya na matatizo ya wananchi yanakuwa yale yale.
“Nitawaita pamoja na viongozi wenzangu kuanzia mkoani hadi wilayani , mtuambie mwelekeo wa matatizo ya wananchi mliyoyasikia na namna mlivyowasaidia, illi sisi viongozi tuyajue na tuweze kusonga mbele na sio kila anapokuja kiongozi mpya mwananchi anarudia tatizo lile, mkifanya kazi yenu kwa umakini hayo hayatakuwepo, “ alisema Mhe Mtaka.
Amesema Serikali iliamua kuwapa majukumu hayo wasaidizi wa kisheria kwa kuwa ni watu ambao wanakutana na wananachi katika shughuli zao za kila siku na hivyo ni jukumu lao kuwajulisha viongozi wao juu ya kile kinachoendelea miongoni mwa wananchi na namna wanavyoyatatua matatizo ya wananchi.
Wasajili wasaidizi msaada wa kisheria ni maafisa maendeleo ya jamii kutoka katika mikoa, miji, majiji na halmashauri za wilaya nchini kote na wamekasimiwa mamlaka ya kuratibu na kusajili wasaidizi wa sheria na taasisi zinazotoa huduma za msaada wa sheria kwa wananchi nchini kama ambavyo Sheria ya Msaaada wa Sheria Na. 1 ya mwaka 2017 iliyoanza kutumika nchini Julai Mosi 2017 inavyosema.
Kupitia Sheria ya Msaada wa Sheria, Wizara ya Katiba na Sheria inafanya kazi kwa ukaribu na wasajili wasaidizi hao na kuhakikisha huduma za msaaada wa kisheria zinapatikana nchini kwa kila mwananchi mwenye uhitaji na ambaye hana uwezo wa kulipia huduma zinazotolewa na mawakili nchini.
Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na wasajili wasaidizi mkoa wa Simiyu inashiriki maonyesho ya wakulima ya Nane Nane mjini Bariadi ambako elimu juu ya sheria mbalimbali na msaada wa sheria vinatolewa bure kwa wananchi wanaotembelea banda la Wizara kwa kushirikiana na Wasajili Wasaidizi hao.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments