WATAALAMU MBINGA,NYASA ,NAMTUMBO NA SONGEA KUPIGWA MSASA | ZamotoHabari.

NA YEREMIAS NGERANGERA…SONGEA

Wataalamu 14 kutoka kila halmashauri za wilaya ya Mbinga ,Nyasa,Namtumbo pamoja na Songea Mkoani Ruvuma wanapatiwa mafunzo ya namna ya kutengeneza mpango wa taifa wa matumizi bora ya ardhi katika HaLmashauri na wilaya zao

Mafunzo hayo yanafanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa chuo kikuu cha Ajuco kilichopo manispaa ya songea ambapo jumla ya wataalamu 56 kutoka katika Halmashauri hizo wanapatiwa mafunzo hayo

Aidha mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia program ya Mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu{FORVAC}forest and value added chain na pamoja na serikali ya Finland,

Wawezeshaji katika mafunzo hayo ni Alex Njahani meneja wa program ya Mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu kutoka Dar..es..salaam ,Emmanuel Msofe mratibu wa program ya Mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu.

Wataalamu kutoka katika Halmashauri na wilaya akiwemo Kelvin Mnali kutoka halmashauri ya Namtumbo na Maurus hyera kutoka Halmashauri ya mbinga walidai mafunzo hayo yatawasaidia namna ya kupeana uzoefu wa kutatua changamoto zinazojitokeza katika upangaji wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji ili kuondoa migogoro baada ya kuzalisha migogoro baada ya mpango kukamilika,

Jumla vijiji 12 mkoani Ruvuma vinatarajiwa kuingia katika mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kutengeneza mnyororo wa kuongeza thamani kwa mazao ya misitu FORVAC ambapo Mbinga vijiji 3,Nyasa vijiji 3,Namtumbo vijiji 3 na Songea Vijiji3 na kufanya jumla ya vijiji 12.
Endrew Ferdinand aliyeinua mikono katikati akitoa ufafanuzi wa namna ya uchoraji wa ramani za vijiji vilivyoomba kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi kwa wataalamu Mkoani Ruvuma katika ukumbi wa AJUCO manispaa ya songea naAndrew ni mtaalamu wa maswala ya ramani FORVAC 


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini