Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania (JDU), Mhe. Zahra Maruma (wa kwanza kushoto) akielezea jambo kuhusu baadhi ya watumishi watakaofanya kazi katika Mahakama Inayotembea kwa ujumbe kutoka Benki ya Dunia. Wajumbe ni (katikati) Deborah Isser na Waleed Malik (kulia).(Picha na Aziza Muhali, SJMC)
Wajumbe kutoka Benki ya Dunia ukiendelea kufanya kikao na watumishi hao.
Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, Waleed Malik akielezea kuhusu matumizi ya vipeperushi kama njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya Mahakama Inayotembea.
Na Aziza Muhali (SJMC)
Watumishi wa Mahakama ya Tanzania watakaofanya kazi katika Mahakama Inayootembea ‘Mobile Court’ katika jijini la Dar es Salaam, wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi katika mazingira mapya ya Mahama hiyo, ili kutoa huduma bora za kimahakama.
Akizungumza leo Agosti 30, mwaka huu katika ukumbi wa kufanyia mikutano Kitengo cha Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania (JDU) , Mtaalam kutoka Benki ya Dunia (WB),Waleed Malik amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali nyadhifa za utumishi wao,
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa si mtu mmoja atakaye husika katika utendaji kazi wa Mahakama hiyo , bali jopo la watumishi , ambapo aliwataja baadhi yao akiwemo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Karani, Afisa Habari, Katibu Mahususi, Mtaalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dereva.
“Mnatakiwa kuwa tayari kupata taarifa za ghafla ambazo zitawataka kufanya maboresho katika utendaji kazi wenu, na namna ya kutatua matatizo ya ghafla yanayotokea katika vifaa vinavyotumika kufanyia kazi ndani ya Mahakama hii kutoa taarifa na kupokea taarifa kwa umma juu ya ufanisi wa utendaji kazi”, alisema Waleed.
Waleed alifafanua kwamba wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kuleta matokeo chanya juu ya Mahakama hiyo na faida kwao katika utendaji kazi.Aliongeza wanatakiwa kuendelea kutoa elimu na kutoa vipeperushi kuhusu Mahakama hiyo, ili wananchi wapate kuilewa na kupata huduma mbalimbali.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments