"ADHABU ZA SHULENI NI ADHABU ZA UPENDO";PADRI JISO | ZamotoHabari.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

“ADHABU mnazopewa shuleni ni adhabu za upendo, zinalenga kuwarekebisha ili akili ziweze kupokea maarifa mnayopewa na walimu na hatimaye muwe raia wema wenye uwezo wa kuztumikia taifa na jamii, tofauti na adhabu mtakazopewa baada ya kumaliza elimu, huko mitaani mtakutana na adhabu za chuki zinazotokana na maarifa kidogo mliyonayo.” Hayo ni maneno yaliyosemwa na Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa mahafali ya saba ya darasa la saba shule ya Carmel Convent iliyoko Vikindu, Wilayani Mkuranga

Padri Jiso ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ambayo ni ya saba kufanyika katika shule hiyo, aliwaasa wanafunzi kuendeleza yale mema waliyojifunza katika kipindi cha miama saba waliyokuwa shuleni.

Alisema binadamu wametunukiwa zawadi kubwa na Mwenyezimungu ya kutumia maarifa na akili katika kuyatawala mazingira, licha ya kwamba sayansi inaonyesha miaka mingi ya nyuma binadamu ambaye yuko katika kundi la wanayama, na kama walivyo wanayama wengine aliishi porini.

“Lakini kutokana na upendo wa Mungu, alituongezea maarifa na vipaji mbalimbali vilivyotuwezesha kutawala mazingira kwa manufaa yetu na viumbe vingine ndio maana leo hii binadamu licha ya kutokuwa na maguvu kama walivyo wanyama wengine Tembo na Simba tumeweza kujenga majumba kuishi kwenye mazingira mazuri na yakliyo bora, kupata huduma za afya na elimu.” Alifafanua na kuongeza Tembo na mahguvu yake, Simba na magubvu yake wao bado wako pori ni na hawajabadilika kwa miaka yote hiyo.

Alitoa mfano wa ndege aitwaye Tai (Eagle) ambaye ana nguvu nyingi, kucha kali zenye uwezo wa kuchakura na kupokonya, mdomo wenye chongo kali na anakadiriwa kuishi hadi miaka 50, lakini watafiti wengi wanase kabla ya kufikisha miaka hiyo 50 Tai ama Eagle hufa kabla ya kufikisha umri huo kutokana na viungo vyake vinavyomuwezesha kupata chakula, kutishiwa nguvu hizo, kwani nkucha hupinda na hivyo hushindwa kupokonya na kuchakura vyakula, mdomo nao hupinda na hivyo uwezo wake wa kudonoa nao hupungua na hatimaye hufa kwa sababu hawezi tena kujitafutia chakula.

“Hii ndiyo tofauti ya wanyama wengine na binadamu kwani sisi tumejengewa maarifa kwa hivyo tunatumia maarifa hayo kutatua kero mbalimbali na hivyo kishi kwa furaha.” Alisema Padri Jiso.

Kwa kutumia mfano huo Padri Jiso alisema ndio maana watoto hujengewa msingi mzuri wa maarifa kwa kupatiwa elimu ili hatimaye baadaye waweze kutawala mazingira wanayoishi kwa kuwa wananachi wazuri na wenye faida kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Padri huyo aliwaonya wanafunzi hao kuwa lazima watambue, adhabu walizokuwa wanapata wakiwa shuleni ni adhabu za upendo zilizolenga kuwarekebisha ili kujaza maarifa kwenye vichwa vyao kwa faida ya baadaye na kwamba nje ya mazingira ya shule adhabu wataakazopata ni za “chuki” na hazina upendo wowote zaidi ya kuwuadhibi ili kuleta majuto.

Katika mahafali hayo pamoja na mambo mengine, wanafunzi walikabidhiwa vyeti (Living certificates) na kushuhudia burudani mbalimbali zilizoporomoshwa na wanafunzi wenzao.Mtihani wa taifa wa darasa la saba unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia Septemba 11, 2019.
Mlulu Khalfan Said (kulia), akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (Darasa la VII) kutoka kwa Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa sherehe za Mahafali ya Saba Shule ya Carmel Convent iliyoko Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani Agosti 31, 2019.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini