Aliyewai Kuwa Kocha wa Taifa Stars afariki Dunia | ZamotoHabari.

Kocha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mjerumani Rudolf ‘Rudi’ Gutendorf  amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 93 jana.

Taarifa ya familia yake nchini Ujerumani imesema kwamba Gutendorf aliyeweka rekodi ya dunia ya kufundisha timu nyingi zaidi duniani, 55 katika nchi 32 za mabara matano amefariki dunia jana.
Makamu wa Rais wa Chama cha Soka Ujerumani, Dk Rainer Koch alimpe heshima ya “Balozi Bora wa Soka ya Ujerumani”.

Kwa mara ya mwisho Gutendorf alifundisha kikosi cha timu ya taifa ya Samoa mwaka 2003 baada ya kuweka pia rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kutwaa taji la Ligi Kuu ya Japan mwaka 1984 akiwa na klabu ya Yomiuri SC.

Nchini Tanzania atakumbukwa zaidi alipoiwezesha Bara kufika fainali ya michuano hiyo mwaka 1981  mjini Dar es Salaam na kufungwa na Kenya Novemba 28, bao pekee la James Ouma dakika ya 22.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini