ASASI ZA KIRAIA ZINAITAKA SADC KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA JUU YA UKATILI UNAOENDELEA AFRIKA KUSINI. | ZamotoHabari.

ASASI ZA KIRAIA WANACHAMA WA TANGO, TUCTA NA CCT INAITAKA SADC KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA JUU YA UKATILI UNAOENDELEA NCHINI AFRIKA KUSINI.

Kuibuka kwa ukatili wa hivi karibuni nchini Afrika Kusini ni suala la kutia huzuni kubwa kwa nchi hiyo, kanda yote ya SADC na bara la Afrika kwa ujumla. Kwa bahati mbaya mashambulizi haya yaliyolengwa dhidi ya watu wanaotazamwa kama “wageni” sio matukio ya nadra yanayofanywa na
wahalifu wachache. 

Sasa ni wazi bila kupinga kuwa hali ya kibaguzi dhidi ya waafrika wenzao imeongezeka miongoni mwa raia nchini Afrika Kusini, jambo ambalo linakinzana na Sera za SADC zinazohimiza umoja, ushirikiano, usalama na uhuru wa raia kusafiri na kufanya shughuli za kiuchumi
katika nchi wanachama ili mradi wanazingatia sheria na taratibu zilizokubalika ndani ya SADC.

Inafikirisha pia kuwa vyama vya siasa nchini Afrika Kusini, karibu vyote, vimekuwa vikifungamana nahisia finyu, kejeli na zisizo-sahihi za utaifa kitu ambacho sio tu kinahalalisha uvunjaji haki na utengano bali kinatanua wigo wa chuki na ubaguzi. Ni wazi pia kuwa watu maskini nchini Afrika Kusini
wanapata tabu kwa kukosa kuthaminiwa, haki za binadamu na fursa za kujiendeleza kibinafsi. 

Tofauti zinazosababishwa na mfumo kati ya walionacho na wasionacho nchini humo inakuza saikolojia ya ukatili ambayo jamii nchini humo bado haijaishughulikia kwa zaidi ya miaka 20 tangu nchi hiyo ianze
kuwa na mfumo wa utawala wa walio wengi. 

Ukatili ulioenea na kulindwa kimfumo nyakati za Ubaguzi wa Rangi (Apartheid) na Ukoloni haujatafutiwa ufumbuzi wa kutosha na serikali ya kidemokrasia. Ukatili wa kila siku unaowakumba watu wengi waishio nchini Afrika Kusini – ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaume; ubaguzi wa kimfumo na kijinsia; ubaguzi wa makundi fulani kijamii - na ukatili dhidi ya maskini na kwa wale waliotengwa kijamii unaleta muunganiko ulio wazi na unachangia kuwaweka kafara Waafrika wengine kwa mateso na kero za watu maskini nchini humo.

Kwenye mkutano wetu wa hivi karibuni wa Jukwaa la AZAKI za SADC jijini Dar es Salaam, Tanzania –vyama vya wafanyakazi, AZISE, asasi za kidini za ukanda huo – zilitamka wazi: “Mkutano wa 15 wa Jukwaa la AZAKI unatanabahisha na kutahadhalisha ukatili unaondelea kwa raia/watu wa mataifa mengine, hasa nchini Afrika Kusini. 

Tunalaani mashambulizi hayo na kwa mara nyingine kuzitaka nchi
wanachama wa SADC kulaani kwa pamoja matamshi na mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni yanayoendelea nchini Afrika Kusini. Serikali ya Afrika Kusini na nchi nyingine wanachama za SADC, lazima zihakikishe usalama na kuthamini haki za binandamu za raia wote wa nchi nyingine wanaoishi
ndani ya mipaka ya nchi hizo.” (Agosti 15, 2019 Tamko la Jukwaa la AZAKI la SADC CSF).

Namna ambavyo ukatili huu wa hivi karibuni kabisa uliovyoandaliwa ni jambo la kutisha, ikiashiria ongezeko la kuwalenga watu ambao sio raia wa nchi hiyo.

 Dola nchini Afrika Kusini, wadau wengine na serikali lazima wakomeshe ‘ukanaji’ wa haki za binadamu kwa wageni ambao unaoneshwa na ukatili huu na watambue kuwa vitendo hivi vya kihalifu na udhalilishaji sio vya kuzuka, au vya nadra, kwa hakika hivi ni vitendo vya kupangwa vinavyotokana na chuki, umaskini na kukata tamaa ya maisha. 

Suala hili halina budi kuwekwa kwenye ajenda ya SADC ili kuisaidia Jamhuri ya Afrika Kusini kuweza kuingilia kati hali hii. Ni budi pia kuwakemea viongozi waliotamka kuwa'waliofanywa haya
wana upungufu wa akili' kwani kukubali mtazamo huo ni kukubali kutawaondoa wahalifu dhidi ya kuchukuliwa hatua za kuwashtaki mahakamani kwa makosa ya jinai kwa kudhaniwa tu kuwa ni
wendawazimu.

Pia kumewepo na matukio ya wanawake na wasichana kubakwa wakati vurugu, mashambulizi na ukatili huu ukiendelea. Huu ni ukikwaji mkubwa sana wa haki za binadamu. Tunatarajia hili likemewe kwa nguvu zote na SADC na kuitaka Serikali ya Afrika Kusini iombe radhi hadharani juu ya vitendo hivyo viovu hususan vya ubakaji na makosa yanayofanana na hayo yaliyofanywa kwa wanawake bila kujali rangi au utaifa wao.

AZAKI za Tanzania pia zinaitaka serikali ya Afrika Kusini na uongozi wa Jumuiya ya SADC kuhakikisha kuwa waliotekeleza mashambulizi na uhalifu huu wa kijinai wanatiwa nguvuni na kuchukuliwa hatua stahiki kisheria.
Baraza la Mawaziri la SADC linalohusika na Chombo cha Siasa, Ulinzi na Masuala ya Usalama lazima washtushwe na ukatili ulioikumba Afrika Kusini na kukutana haraka ili kupata taarifa ya uchunguzi wa kina kutoka kwa Serikali ya Afrika Kusini, waunge mkono juhudi na kukubaliana juu ya aina ya msaada unaotakiwa kutolewa kwa raia wa nchi za SADC na Afrika waliomo ndani ya mipaka ya nchi hiyo.

Tunaitaka serikali ya Afrika Kusini kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia wa kigeni pamoja na mali zao.

TANGO, TUCTA na CCT inaziomba kwa heshima na taadhima Serikali za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Zimbabwe kuchukua hatua stahiki za kiuongozi ndani ya SADC kuhakikisha suluhisho la haraka linapatikana. TANGO, TUCTA na CCT ziko pamoja na AZAKI ambazo juhudi zake za kuzuia,
kupatanisha na kuhudumia wahanga wa ukatili huo na kwa mshikamano na ndugu zetu wake kwa waume nchini Afrika Kusini na kuwahakikishia mfungamano wetu kamili kwenye juhudi hizo.

Tunatoa rai kwa Rais wa Afrika Kusini kukutana na wawakilishi wanaohusika kwenye jamii zilizoathiriwa na kukemea waziwazi ubaguzi na chuki dhidi ya wageni, kuweka mazingira ya kuwarejeshea maisha yao wahanga wa ukatili huu na kurejelea ahadi ya kukomesha kutokea tena kwa
mashambulizi haya kwa wasio-raia wa Jamhuri ya Afrika Kusini.

TANGO ni shirika mwavuli la asasi za kiraia nchini lililodumu kwa muda mrefu na kubwa zaidi Tanzania likiwa na dhamana ya uwakilishi wa mashirika zaidi ya 600 hapa nchini.

 Wanachama wa TANGO ni pamoja na mitandao ya kimkoa na kiwilaya ipatayo 28 na AZAKI moja moja; TANGO ina utajiri wa utofauti, upana na ujumuishi wa AZISE/AZAKI zinazofanya kazi kwenye sekta za ardhi, mazingira, madini, elimu, afya, kilimo, utamaduni, uwezeshaji kiuchumi, wanawake, watoto, vijana, wazee, watu wenye ulemavu na wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi (VVU).


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini