Hatana mashaka hata kwa uchache katika upana wa uimbaji na utunzi wa Baraka Da Prince. (Mjuzi)
Baraka toka yake ni ya upekee mno, hakuwa na muigo wa msanii yoyote kama awali za wengi. (Muziki)
Juzi, jana ya Baraka Da Prince ilikuwa ni katika mvumo mzuri mno. Maanishio letu ni Siachani Nawe, Nivumilie, Jichunge lakini Sina. (Nyimbo)
Na nyakati hizo ikumbukwe hakuwa pekee bali watu wenye kumuongoza vyema. Pia ifahamike “Wawili ni wawili tu” (Mawazo)
Leo ya Baraka ni katika anguko kuu, na uhalisia si kama hana uwezo wa kipawa, hapana bali mikakati katika upana wa soko. (Uongozi)
Baraka anahitaji kuwa na mtu ama watu katika ongoza yake. Na watu wawe ni wenye mikakati ya namna ya kuweza kumuweka Baraka sokoni. (Biashara)
Ikumbukwe “Kuimba ni mosi, biashara ni pili” Na daima biashara inahitaji wajuzi wenye ujuzi haswa. (Ufahamu)
Vivyo kama Baraka ataendelea kujiongoza mwenyewe ni wazi anguko lake ni endelevu katika soko. (Uhalisia)
Lakini akiwa chini ya genge la wajuzi hakika Baraka ni biashara yenye upekee katika soko hili la muziki. (Hakika)
Na yeye anaweza pinga kwa ukubwa kweli hii, lakini haiwezi kutushangaza yakuwa “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” (Tafakari)
By Tizneez
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments