MWANDANI wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch, anatarajiwa kujifungua muda wowote kuanza sasa.
Lakini akiwa kwenye hali hiyo, Tanasha ameeleza hali inayompata sasa hivi ya kwenda haja ndogo kila baada ya dakika kumi, ishu ambayo daktari wa gazeti hili ameifungukia.
Kupitia ‘statas’ yake ya ukurasa wa Instagram, Tanasha aliwashirikisha mashabi wake hali yake hiyo, lakini akasema anaifurahia.
“Nipo kwenye hatua ambayo ninakwenda haja ndogo kila baada ya dakika kumi. Ni usumbufu, lakini ninafurahia,” aliandika Tanasha ambaye ni mtangazaji wa redio nchini Kenya.
Ili kujua undani wa hali hiyo na kama ni tatizo kubwa kwa mjamzito, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilizungumza na daktari wake, Godfrey Charles ‘Dk Chale’ ambapo alieleza undani wa hali hiyo.
“Katika kipindi cha mwanzo, yaani miezi ya awali ya ujauzito, kunakuwa na mkandamizo unaotokana na ukuaji wa kiumbe kilichoko tumboni. Hali hii husababisha mfuko wa mtoto kusukuma kibofu cha mkoji ili uzidi kuchukua nafasi ya utanukaji wake.
“Sasa, hali hiyo hufanya kibofu kujaa mkojo kwa urahisi na kushindwa kuhifadhi kiasi kikubwa cha mkojo.
“Kitendo hicho ndicho husababisha mama kupata mkojo mara kwa mara kutokana na kichwa cha mtoto kukandamiza kibofu.
“Kwa ushauri tu ni kwamba huyo mjamzito ahakikishe kila anapohisi mkojo, basi aende haja ndogo bila kujali kama ni mara kwa mara.
“Anapaswa kuhakikisha haruhusu kubana mkojo kwa muda mrefu kwa sababu akifanya hivyo inaweza kumsababishia kupasuka kwa kibofu cha mkojo au kupata maambukizi kwa njia ya mkojo.
“Hata hivyo, mama mjamzito anapopata maumivu wakati wa kukojoa ni vyema kumueleza daktari wake ili aweze kupata msaada zaidi wa kitaalam na si kweli kwamba jambo hilo ni ugonjwa mkubwa kama baadhi ya watu wanavyofikiria,” alisema daktari huyo.
Wataalam wengine walisema kuwa huenda Tanasha anapitia kwenye hali hiyo kwa kuwa huo ni ujauzito wake wa kwanza
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments