Mchezaji wa kimataifa wa Iran mwenye asili ya Sweden Saman Ghoddos, amefungiwa kucheza soka kwa muda wa miezi minne na Shirikisho la soka duniani (FIFA) kutokana na kushindwa kuheshimu makubaliano aliyofikia ya kujiunga na klabu ya SD Huesca.
Huesca iliyopanda ligi kuu ya Uhispania (La Liga) inadai kuwa, walishafikia makubalinao ya kumnunua Ghoddos kutoka klabu yake ya Sweden na kwamba mchezaji huyo alishasaini mkataba.
Kamati ya utatuzi migogoro ya FIFA imebaini kuwa klabu hiyo ya Uhispania ilikuwa sahihi, mbali na kumfungia Ghoddos, FIFA imemtaka pia mchezaji huyo kuilipa fidia klabu hiyo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments