Facebook inavyotumika kufanya biashara ya wanyamapori nchi za Asia | ZamotoHabari.


Na Bakari Kimwanga -Aliyekuwa Thailand

TANZANIA ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizobarikiwa kuwa na wanyama wa aina mbalimbali, ambapo katika kuhakikisha utulivu unapatikanakwenye hifadhi, Serikali imekuwa ikitunga sheria mbalimbali kwa lengola kulinda rasilimali hiyo muhimu.

Katika uso wa dunia, Tanzania inatajwa kuwa nchi iliyofanikiwa
kudhibiti biashara ya wanyama kwa kuwa na sheria kadhaa zinazozilinda
hifadhi.

Wizara ya Maliasili na Utalii, imepewa jukumu la kutayarisha sera ya
wanyamapori, kusimamia utekelezaji wake na kuratibu maendeleo ya
sekta ya wanyamapori nchini.

Sera ya wanyamapori inaeleza kwamba matarajio ya sekta hiyo miaka 20
ijayo ni kwenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.
Kwa hapa nchini, historia ya uhifadhi wa wanyamapori inarudi nyuma
hadi mwaka 1891 wakati sheria ya kudhibiti uwindaji ilipoanzishwa na
utawala wa Wajerumani.

Sheria hizi zilidhibiti uvunaji wa wanyama; mbinu za uwindaji na
biashara ya wanyamapori, ambapo baadhi ya aina ya wanyama waliokuwa
hatarini kutoweka walilindwa ipasavyo. Hifadhi za kwanza za
wanyamapori, zilianzishwa na Wajerumani mnamo mwaka1905 katika eneo
ambalo sasa linaitwa Pori la Akiba la Selous.

Maeneo ya kuhifadhi wanyamapori yalichaguliwa kutokana na kuwapo kwa
wanyama wakubwa, na wala si kwa sababu za makundi anuwai ya
kibaiolojia.

Wanyamapori wa Tanzania ni urithi wa asili wa pekee na rasilimali
yenye umuhimu mkubwa kitaifa na kimataifa. Umuhimu wake umejikita
katika thamani ya kibaiolojia ya spishi zenyewe na mazingira ya asili
yaliyopo nchini, thamani yake ya kiuchumi na uwezo wake katika
kuchangia maendeleo endelevu nchini.

Kupitia sheria zilizopo za uhifadhi wa wanyamapori kama vile Sheria ya
Uhifadhi wa Wanayamapori Na12 ya mwaka 1974, Sheria ya Hifadhi ya
Ngorongoro Kifungu cha 413 ya mwaka 1959, Sheria ya TANAPA kifungu cha
412 ya mwaka 1959 na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori
Serengeti ya mwaka 1980 zinaweka mkazo katika kulinda rasilimali za
wanyamapori.

Kutokana na muhimu huo, hivi karibuni Chama cha Waandishi wa Habari za
Mazingira Tanzania (JET), kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la
RTI ambao wanatekeleza mradi wa usafirishaji haramu wanyamapori chini
ya USAID Protect, iliwakutanisha waandishi wa habari wa Tanzania na
Thailand, ambayo ni moja ya nchi za Kusini mwa Asia inayotajwa kuwa na
kiwango kikubwa cha wanyama wanaopita nchini humo kutoka nchi za
Afrika kwenda mataifa mengine.

Wanahabari hao kutoka nchi hizo kila upande waliweza kubadilishana
uzoefu na taarifa za kina kuhusu usafirishaji haramu wa wanyamapori
ambapo kila upande waliweza kwenda kwa nchi husika na kujifunza na
hata kuona hali halisi ya ulinzi wa hifadhi za taifa.
Ripoti ya Traffic ya mwaka 2018 iliangazia tathmini ya haraka kuhusu
utumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facebook kama kiunganishi cha
biashara ya wanyamapori nchini Thailand.

Ripoti hiyo pia ilichapishwa katika mtandao wa Thailand 24 Traffic kwa
ajili ya ufuatiliaji biashara ya wanyamapori.

Ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ulimwenguni kote
katika biashara ya wanyama wa porini na mimea kwa muktadha wa uhifadhiwa biolojia wa aina zote na maendeleo endelevu.

Katika ripiti hiyo mpya ya Traffic, inaelezwa kuwa mamia ya wanyama
hai wa porini wanauzwa kupitia mtandao wa Facebook nchini Thailand,
bila usajili kwa sababu wao sio wa asili ya nchi hiyo.

Wanyama wengi wanaouzwa walikuwa watoto wachanga, waliopewa dhamana yabiashara ya wanyama. Karibu nusu ya aina ya wanyama wanaopatikanakatika biashara hiyo, asilimia 47 bado hawajapewa ulinzi chini yasheria ya msingi ya wanyamapori ya Thailand, Sheria ya Hifadhi ya
Wanyama wa Porini na Sheria B. 2535 (WARPA) nyingi kwa sababu sio wa
asili ya nchi hiyo.

Wanyama hao, Black Pond Turtle Geoclemys hamiltonii, ambao si wa
asili, wameorodheshwa katika taarifa ya CITES na ni marufuku kufanyika
kwa biashara hiyo, lakini mara kwa mara hubebwa nchini humo.

Hivi sasa, ni aina 12 tu ndio sio wa asili wakiwamo mamalia saba,
ndege moja, reptilia watatu na kipepeo mmoja, wanaolindwa chini ya
Sheria ya WARPA. Aina 200 zilizorekodiwa na utafiti wa Traffic
zilikuwa na mamalia, ndege na wanyama watambaao.

Kukua kwa biashara ya wanyamapori mtandaoni kumeongoza zaidi kwa ainazisizo za asili ambazo kwa sasa hazina kinga ya kisheria au kanuni.

Kaimu Mkurugenzi wa Mkoa wa Traffic Asia ya Kusini, Kanitha
Krishnasamy, anasema ipo haja ya kuwapo kwa sheria ili kulinda haki za
wanyama na kukomesha bishara hiyo.

“Kupeana aina za ulinzi chini ya sheria za Thailand na kuwezesha
watekelezaji kuchukua hatua, ndiyo njia nzuri zaidi ya kushughulikia
tatizo hili katika sekta ya hifadhi,” anasema Krishnasamy.



BIASHARA INAVYOFANYIKA

Tathmini ya haraka juu ya utumiaji wa Facebook kufanya biashara ya
wanyama wa porini nchini Thailand, inaonesha kuwa nchi hiyo inajitolea
kwa hali na mali kukabiliana na ujangili wa wanyamapori kupitia
Kitengo cha Hawk cha Pori chini ya Idara ya Hifadhi za Taifa,
Wanyamapori na Uhifadhi wa Mimea (DNP).

Hata hivyo, bado inaonyesha kuna mianya ya kisheria inayodhoofisha
juhudi hizi na kuweka spishi zisizo za asili hatarini.

Aidha, ripoti hiyo inaeleza namna ambavyo waandishi wanavyotaka
marekebisho ya sheria na kuwasihi viongozi kuongeza juhudi zao katika
utekelezaji kwa kufanyakazi karibu na Facebook kama njia ya kukuza
mikakati ya pamoja ya kushughulikia biashara haramu ya wanyamapori
mitandaoni.
Biashara haramu ya wanyamapori nchini Thailand, inayojumuisha aina za
asili na zisizo za asili, inajumuisha ununuzi na uuzaji wa wanyama hai
katika masoko maarufu ya wikendi na Chatuchak.

Njia hii ya kufanya biashara mtandaoni inazidi kushamiri ulimwenguni
na wakati mwingine ni matokeo ya kuhamishwa kutoka masoko ya asili
kwenda mtandaoni.

Utafiti uliofanywa nchini Malaysia juu ya biashara ya torto na turtle
za maji safi ulipata mabadiliko makubwa katika mifumo ya biashara,
mfano kuhama kutoka kwa mtandao wa kijamii (Bouhuys na van
Scherpenzel).

Mfano, nchini Thailand Facebook ni maarufu na mtandao wa Thais.
Mitandao ya kijamii umeona ukuaji mkubwa wa watumiaji nchini Thailand
baada ya 2010 na sasa inafanya kazi kama mtandao mkubwa zaidi wa
kijamii na jukwaa la biashara nchini humo.

Biashara haramu ya wanyama pori pia hufanyika, ambapo inaripotiwa
kuwa wafanyabiashara kadhaa wamekamatwa na vyombo vya kutekeleza
sheria.

Desemba 2015, viongozi wa Thailand waliripoti kwamba watuhumiwa wawiliambao walikuwa wakitangaza Burmese Star Tortoises Geochelone platynotaya kuuza kupitia Facebook walikamatwa. Turmese Star Burmese ambao sioasili ya Thailand na ni aina ya sambayo, hupimwa ulimwenguni kote kamailivyowekwa hatarini na IUCN1.



KAULI YA KIKOSI KAZI

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi Kazi cha Ulinzi wa Wanyamapori Ofisi ya
Hifadhi ya Wanyamapori, Thiradej Palasuwan, anasema wamekuwa
wakipambana kupitia kikosi kazi na watu wanaofanyabishara hiyo haramu
ya wanyamapori.

“Kwa mfano hapa kuna mtu alijitambulisha anaitwa kina kwenye Facebook
akiwa anauza wanyama, lakini tulipofanya uchunguzi tuliweza kubaini ni
mtu mzima, na tulifanikiwa kumtia mbaroni kwa mujibu wa sheria za
nchi.

“Haya ni mapambano ambayo hatuchoki na kubwa tunawataka wanahabari
muendelee kuwafichua watu hao ambao wamekuwa wakifanya hii biashara,”anasema Palasuwan.


RIPOTI YA INTERPOL

Katika kukuza na kuunga mkono utekelezaji wa mapambano hayo, Interpol
nchini Thailand imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali katika
uhalifu wa wanyamapori na hatari ya baonuai.

Kikosi hicho kimekuwa kikibadilishana taarifa mbalimbali na nchi
wanachama kuhusu mtandao wa biashara hiyo, malengo na kuchunguza kwakina na hatimaye kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa.






Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini