Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33), mwenye wake watu na watoto sita amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na wake zake wawili katika kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Mbali na Mchungaji Chirhuza, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Esther Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) ambao ni wake wa mchungaji huyo na Samwel Samy (22) ambaye ni mdogo wa Mchungaji huyo.
Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Mbando na kusomewa mashtaka mawili ya kuishi nchini bila vibali. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 9 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments