Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Uhaba wa wafanyakazi katika katika kituo Cha afya Cha muriet kilichopo jijini Arusha Bado ni changamoto kubwa inayoikabili kituo hicho .
Akizungumzia swala hilo mganga mkuu wa jiji la Arusha Dr Simon Chacha wakati akisoma historia ya kituo hicho mbele ya katibu mkuu wa ofisi ya Rais (TAMISEMI)mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema kuwa kituo hicho Bado Kina changamoto ya wafanyakazi .
Alisema kuwa kituo hicho kina jumla ya wafanyakazi 25 na kuna uhitaji waambao ni wachache sana na hawatoshi kwani walitakiwa watumishi 52 katika kila kituo Cha afya .
Chacha ameendelea kusema kuwa katika kituo hicho Bado pia wanauhitaji wa vifaa vya matibabu ikiwa baadhi ya vifaa wamevipata kwa kupitia mfuko wa ndani ya jiji katika mapato pia kwa kuwezeshwa na wawekezaji ikiwa mkuu wa mkoa na wengine.
Alisema kuwa ujenzi wa Kituo hicho kimegarimu kiasi cha shilingi billion 1 na elfu 59 ambapo halmashauri ilichangia milion 359 na serikali kuchangia milion 700 , huku akibainisha kuwa kituo hicho kinahudumia mitaa 13 ambayo ina wakazi wasiopungua elfu 50
Aidha alitaja majengo yaliokamilika had I sasa ni pamoja na jengo ya exray, OPD, maabara, jengo la mama na mtoto ,upasuaji pamoja na jengo la kuhifadhia maiti.
Kwa upande wake katibu mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI mhandisi Joseph Nyamuhanga alifurahishwa na Kazi iliofanywa alishukuru halmashauri kwa kununua vifaa vya utendaji kazi katika kituo hicho pia alisema kuwa wao kama serikali watahakikisha wanapata vifaa pamoja na kuleta watumishi ili waweze kufikia idadi inayotakiwa ili waweze kutoa matibabu mazuri kwa wananchi .
"Tatizo Hilo la uhaba wa wafanyakazi kazi Bado lipo kwenye vituo afya ,zahanati na hospital sisi kama serikali tutajitahidi kukamilisha idadi ya watumishi hao inaongezeka napenda kumaliza kwa kuwashukuru wafanyakazi wa kituo hichi kwa kuendelea kufanya kazi kwa umahiri na kuhakikisha wagonjwa wanavutiwa na huduma yenu " alisema Nyamuhanga
Akizungumza meya wa jiji kalist Lazaro amesema kuwa anamshukuru Sana katibu mkuu kwa kutembelea kituo hicho ba kuendelea kusema halimashauri yao itakapokuwa na uwezo hawatasubiri kufanya maendeleo ili kuwasaidia wananchi wake.
"Tunahitaji kufanya maendeleo Kama halmashauri ili kuipunguzia serikali mzigo napenda kusema Mimi na mkurugenzi wa jiji tunaendelea kushughulikia miradi ili kuinua maendeleo katika mkoa wetu " Lazaro.
Picha ikionesha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI mhandisi Joseph Nyamuhanga akizungumza na Wanahabari wakati wa ziara
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments