Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba, amemjia juu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na kumjulisha kuwa ana faili lake linajaa kabati tangu ateuliwe na kwamba akichomoa betri atazimia.
Musiba aliandika ujumbe huo jana kupitia akaunti yake ya Twitter na kumtaka Lugola afanye kazi yake kwa mujibu wa miiko na maadili ya nchi, Tanzania ni nchi yetu sote wazee kwa vijana na kwamba aache kutumia serikali kama kivuli cha jimbo.
Aliandika ujumbe unaosomeka hivi :”Namshauri Kangi Lugola akae akijua nina faili lake ambalo linajaa kabati zima tangu ateuliwe, nikichomoa betri atazimia, afanye kazi kwa mujibu wa miiko na maadili ya nchi, Tanzania ni yetu sote wazee kwa vijana , aache kutumia serikali kama kivuli cha jimbo,” aliandika Musiba.
Waziri Kangi Lugola
Jana Waziri Lugola alimuonya Musiba kuacha mara moja mtindo wa kuwachafua viongozi na watu wengine katika mitandao ya kijamii kwa mgongo wa serikali.
Lugola alisema serikali haiwezi kufanya kazi kwa kuwatuma wanaharakati kuwasemea “Serikali ama Rais haimtumi Musiba kuwajengea hofu Watanzania na atachukuliwa hatua,” alieleza Lugola.
Alisema Musiba akiendelea kueleza anatumwa na serikali watamchukulia hatua kali bila kumuangalia usona wala kumuonea huruma.
Baada ya Waziri kutoa maelekezo hayo Musiba alimjibu kuwa yupo tayari kukamatwa lakini hatoacha kusema kweli.
Musiba aliingia katika Twitter yake na kuandika ujumbe huu
“Nimeona clip ya mheshimiwa akinilenga lakini mbona ina kasoro nyingi za kitaaluma huwezi kuonya wanaharakati kisha ukampointi mtu 1, kwamba Musiba stop wengine wakina kigogo 2014 waendelee kumtukana mhe Rais na serikali yake,”
Aliongezea kuwa:
“Namuomba Kangi Lugola aanze kumsaka kigogo 2014 na Asbert Ngurumo kwanza kutokana na matusi na upotoshaji wake kwa serikali yetu, baada ya kuniziba mdomo mimi ambaye ni mtetezi wa nchi dhidi ya vibaraka. Nampenda Rais wangu, naipenda nchi yangu,”
Namshauri Kange Lugola akae akijua nina faili lake ambalo linajaa kabati zima tangu ateuliwe,nikichomoa betri atazimia ,afanye kazi kwa mujibu wa miiko na maadili ya nchi ,Tanzania ni yetu sote wazee kwa vijana,aache kutumia serikali kama kivuli cha jimbo
— Musiba Cyprian Majura (@CyprianMusiba4) September 13, 2019
Namuomba Kangi Lugola aanze kumsaka Kigogo 2014 ,na Asbert Ngurumo kwanza kutokana na matusi na upotoshaji wake kwa Serikali yetu,badala ya kuniziba mdomo mimi ambaye ni mtetezi wa nchi dhidi ya Vibaraka.Nampenda rais wangu,naipenda nchi yangu . pic.twitter.com/AdwTqazyA6
— Musiba Cyprian Majura (@CyprianMusiba4) September 13, 2019
Nimeiona clip ya mheshimiwa akinilenga lakini mbona inakasoro nyingi za kitaaluma huwezi kuonya wanaharakati Kisha ukampointi mtu 1, kwamba Musiba stop wengine wakina Kigogo 2014 waendelee kumtukana mhe rais na serikali yake. pic.twitter.com/zb3LwlWlKg
— Musiba Cyprian Majura (@CyprianMusiba4) September 13, 2019
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments