Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa
Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar hiyo Mhe. Ali Selemani Ali
akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo na viongozi mbalimbali
walipofika katika eneo walilokabidhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo walilokabidhiwa na Serikali yaJamhuri ya Muungano.
Wajumbe wakiangalia ramani ya eneo hilo walilokabidhiwa kutoka kwa mtaalamuwa ardhi.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo walilokabidhiwa na Serikali yaJamhuri ya Muungano.
Muonekano wa sehemu ya eneo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
watakakalijenga Ofisi zake walilokabidhiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Jijini Dodoma.
**************************
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wametembelea kiwanja kwa ajili ya kujengwaOfisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika eneo la Mahoma MakuluJijini Dodoma.
Ziara hiyo pia ilihusisha wataalamu kutoka Serikali hiyo na viongozi mbalimbaliakiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar Mhe. Mihayo JumaNhunga ambaye aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwakabidhi pa kiwanja hicho.
Mhe. Nhunga alisema kuwa SMZ inafarijika kupata kiwanja hicho ambacho kinaukubwa wa hekta 30 na kuwa itaanza haraka ujenzi wa izo uhusiano wa pandembili za Muungano utaendelea kuimarika.
Serikali hizi mbili zina uhusiano na ushirikiano mzuri na tunaona namna Serikaliya Jamhuri ya Muungano ilivyojitoa na kutupatia kiwanja hiki na tunaona thamaniya Dodoma sasa tofauti na zamani hivyo tunaanza haraka ujenzi wa ofisi zetu tuhamie hapa, alisema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Ali Selemani Ali wanashukuru kwa kupata ardhi hiyo na kuwa ina thamani kubwa kwa Serikali yaZanzibar hivyo undugu baina ya pande hizo mbili utaendelea kuimarika.
Mhe. Ali aliahidi kuwa kama Kamati wataishauri SMZ kuanzisha ujenzi wa Ofisi za serikali hiyo kwa kasi ili waweze kuhamia na kuanza shughuli zake katika Jijila Dodoma.Akitoa shukrani zake kwa ujumbe huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu waRais Balozi Joseph Sokoine aliyeambatana na wakurugenzi wa Idara yaMuungano aliwakarisha kuanza ujenzi na kuhamia.
Balozi Sokoine alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kutaimarisha Muungano na undugu baina ya wananchi wapande hizo mbili.
“Tunafarijika sana tunapoona mnafika hapa kwenye kiwanja chenu mara kwamara na kuona namna mtakavyoanza ujenzi na kukamilika kwa Ofisi hizi kutaletaushirikiano mzuri baina yetu sote”. Alisema.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments