Bobi Wine achoropoka mikononi mwa polisi kushiriki tamasha alilopigwa marufuku | ZamotoHabari.


Mwanamuziki ambaye ni Mwanasiasa, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amefanikiwa kutoroka ulinzi mkali wa Polisi uliokuwa ukizingira nyumba yake huko Magere

Inadaiwa kuwa kwa sasa Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki anaelekea tamasha lake alilozuiwa kulifanya huko Busabala kwa kutumia Bodaboda

Mapema leo asubuhi Polisi walizingira nyumba ya Bobi Wine ili kumzuia kushiriki katika tamasha lake la muziki liitwalo ‘Osobola ku Independence’ kwa Kiingereza ‘Independet Day Music Concert’

Kwa mujibu wake Bobi Wine amedai kuwa Polisi walianza kuzingira nyumba yake na ukumbi wa tamasha hilo jana usiku akidai Polisi hao ndio walisema hawana uwezo wa kulinda watu huko Busabala

Aidha, Msemaji wa Polisi, Fred Enanga ameeleza kuwa tamasha hilo haliwezi kufanyika kwa sababu Bobi Wine ameshindwa kutofautisha siasa na muziki
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini