Wakuu habari,
Mimi natofautiana sana na jamii kiujumla kwenye mambo mengi sana, yaani ni ile wanaitaga non-comformist, sema JF nakutana na ma non -comformist wengi tu kama mimi na hilo linanipa faraja
Kuna hili suala la michango ya harusi, sendoff, kitchen party, baby shower hadi birthday siku hizi, naona limeshika kasi sana siku hizi kutokana na magrupu ya whatsapp, ma schoolmate wa msingi, form 4, form 6, chuo na wafanyakazi wenza wote ni kuchangisha tu, hata kama haupo kwenye grupu unatafutwa kwa simu ama facebook
Mi nadhani suala la harusi (achilia mbali hizo sherehe nyingine ndogondogo) sio ishu ya kuchangiwa, mwenyewe kwenye harusi yangu mimi na mweza wangu hatukuchangisha, simaanishi labda tulikuwa na uwezo sana kuigharamia wenyewe, bali haikuwa kubwa
Vitu kama msiba, au matibabu ya mtu wa karibu au ndugu yake ambaye hana uwezo huwa nachangia lakini harusi, sendoff, kitchen party, birthday, sijui zawadi, graduation au nyingine sichangiagi.
Harusi naona zinafanywa kuwa ghali sana ukilinganishwa na maisha ya watu wanavyoishi, mimi nadhani harusi inapaswa kugharimu sio zaidi ya kipato chako cha nusu mwaka at very maximum, yaani hiyo ndio ghali zaidi.
Yaani kama mshahara wako na huyo mtarajiwa wako ni jumla ya laki 6 kwa mwezi harusi yako haitakiwi kuzidi gharama ya milioni 3.6, zaidi ya hapo itakuwa haiendani na nyie, mtakuwa mmejilipua mno au kuchangisha watu kupita kiasi
Harusi hata kama imefikia kuchangiwa basi haitakiwi kuchangiwa sijui na watu weeengi, kama huna uwezo wa kuigharamikia mwenyewe wachangishe watu waliopo kwenye circle yako kama vile marafiki wa karibu na ndugu, na ndio haohao utakaowaalika kwenye sherehe.
Unakuta mtu hamjawasiliana sijui miaka kama 3 au 10 huko, halafu unakuja kuwasiliana nae unataka eti akuchangie harusi ili ufanye sherehe kubwa, aisee mimi naona aibu
By Chinchilla Coat
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments