Ed Sheeran Atajwa kama Mwanamuziki Mwenye Thamani zaidi Uingereza | ZamotoHabari.


Msanii wa muziki kutoka nchini Uingereza, Ed Sheeran ametajwa kuwa ndiye mwanamuziki tajiri zaidi kwenye kundi la watu maarufu wenye umri chini ya miaka 30 nchini humo akiwa na thamani ya paundi milioni 170.

Kuongezeka kwa thamani ya Ed kumejiri mara mbili ndani ya kipindi cha miezi 12 na ndiyo sababu iliyomfanya kumnyang’anya nafasi ya kwanza mwanamuziki Adele.

Katika orodha hiyo sasa nafasi ya pili imechukuliwa na muigizaji wa filamu maarufu ya ‘Harry Potter’ Daniel Radcliffe akiwa na thamani ya paundi milioni 90 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Harry Styles kutoka kwenye kundi la zamani la One Direction, akiwa na paundi takribani milioni 64.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini