Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hawezi kuwasikiliza Mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC kwani anawasiliana na Uongozi uliompa Mkataba
Ni baada ya mashabiki wa Klabu hiyo kulalamika wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayodai yamekithiri ikiwemo kushindwa kupanga kikosi na kukosa mbinu
"Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwa hiyo siku viongozi wakinitaka niwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini." ameeleza.
"Nina uzoefu mkubwa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yeyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids na hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa ila ligi." Zahera alisisitiza.
Baada ya kufungwa na Pyramids FC goli 2-1 kutokea nchini Misri katika dimba la CCM Kirumba Mwanza, Yanga inahitaji ushindi wa magoli zaidi ya mawili ugenini ili kuweza kusonga mbele
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments