Katibu Mkuu CCM akutana na viongozi wa Serikali na Chama Lindi | ZamotoHabari.


Katibu Mkuu wa CCM,  Dkt. Bashiru Ally amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Serikali mkoa wa Lindi, wilaya na Halmashauri zote.

Kikao hiko kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Ndg. Fadhili Juma Mohamed, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Ndg. Abas Matuliko, Wenyeviti na Makatibu wote wa wilaya wa CCM mkoa wa Lindi, Wenyeviti wote wa Halmashauri na Mameya wote wa Halmashauri, Wakuu wa wilaya na Wabunge wote wa mkoa wa Lindi, ambapo viongozi hao wameongozwa na Mlezi wa Mkoa huo Ndg. Zubeir Ali Maulid mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Spika wa Baraza la Wawakilishi.

Katika kikao hiko cha kazi, Katibu Mkuu pamoja na mengine, amewashauri viongozi hao kuendelea kuimarisha mshikamano uliyopo na kutoruhusu mgawanyiko wa aina yoyote hasa tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mapema mwezi Novemba mwaka huu.

Katibu Mkuu, ameyasema hayo akihitimisha ziara yake ya siku tatu Katika Mkoa wa Lindi ambayo imekuwa ziara yenye hamasa na mafanikio makubwa katika kuimarisha umoja, mshikamano na kuwajengea zaidi wanachama na viongozi moyo wa kujitolea.

Katika kikao hiko, wajumbe wametumia fursa hiyo kushauri na kupendekeza mambo mbalimbli ambayo yamelenga katika kujenga na kuimarisha zaidi mshikamamo ndani ya Chama na serikali kwa ujumla ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Wakati huo huo, Ndg. Zubeir Ali Maulid Mlezi wa Mkoa huo na Spika wa Baraza la wawakilishi amemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara yake ambayo kwa kiasi kikubwa imeimarisha zaidi mahusiano baina ya viongozi wa Chama na serikali.

Ziara hii, ni muendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kwa viongozi kuwa karibu na wanachama, kujenga na kuimarisha mahusiano ngazi zote.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini