Naliona anguko la Harmonize tangu kujitoa kwake WCB | ZamotoHabari.


Wanazengo poleni na majukumu nimemfikiria sana huyu dogo naona anapotea vibaya sana na soon tu tutaanza kumsahau kwani jitihada anazozifanya sidhani kama zitazaa matunda.

Hivi kweli kiburi anachopata kwa hela za ukweni kitamfanya awe juu zaidi ya Mondi? Jibu ni hapana siku tu wakiachana na Sara ndo basi tena.

Halafu huyu jembe ni jembe anaweza kustahimili figisu za muziki wa bongo kweli au anampa kiburi dogo kwa sababu yupo kwenye peak?

Watu wanaompoteza dogo wanakosea sana na hawawezi mfikisha dogo popote. Nafikiri watu wabaya kwa Harmonize ni Jembe ni jembe, Zamaradi Mketema, Dully Sykes.

Wanampoteza sana wengi humu wanazungumzia mtoto akikua akajitaftie lakini Harmonize sio mtoto kwa Diamond. Harmonize hakupaswa kuondoka WCB kulingana na hali aliyokuwa nayo zamani na sasa hivi. Ushauri wangu kwa dogo muda anao, arudi tu kuomba yaishe aendelee na kazi WCB.

By Size 96/JF
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini