Aliyekua Mbunge wa singida Mashariki Tundu Lissu amesema, kwa sasa amesitisha mpango yake ya kurejea Tanzania mpaka hapo usalama wake utakapohakikishwa.
Akizungumza katika mahojiano na VOA Swahili jana Jumatano Oktoba 9, Lissu alisema kwa sasa ameshakamilisha tiba, hivo hana sababu ya kiafya ya kuendelea kukaa Ubelgiji haipo tena na kilichobaki ni suala la viongozi wenzake waliopo Tanzania wamuambie kama mazingira ya kiusalama ya yeye kurudi yapo sawa.
Alisema, waliompiga risasi 16 mchana wa saa 7 katikati ya nyumba za Serikali Dodoma, katikati ya kikao cha Bunge, bado wanaitwa watu wasiojulikana.
Alisema, Awali alisema angerejea nyumbani, Septemba 7 mchana kweupe, lakini amelazimika kubadili uamuzi huo kutokana na mazingira ya kiusalama kutokua mazuri.
“Kuna maneno yamekuwa yakijitokeza katika mitandao ya kijamii, kwamba ngoja aje, mara hii hatutakosea hatutakosea shabaha. Na kuna mtu anaitwa Musiba, ametangaza hadharani kwamba Lissu akija atapigwa risasi, katika mazingira hayo, watu wenye busara watasema hebu tuangalie hali ya usalama,” alisema Lissu
Lissu aliongeza kuwa, licha ya yote hayo, hawezi akakwamia ughaibuni, lazima atarudi nyumbani kwani Rais Magufuli hatakuwa madarakani milele.
Kuhusu afya yake kwa sasa, amesema, tanguu tarehe 29 mwezi juni mwaka huu ameacha kutumia magongo, ingawa anachehemea kidogo, anaweza kutembea mwenyewe.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments