Nandy Ahamia Jumba la Kifalme | ZamotoHabari.


ACHANA na madili manono ya ubalozi anayoendelea kutengeneza, sexy lady kunako Muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amehamia kwenye jumba lenye hadhi kifalme maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Risasi Jumamosi lina data kamili.



Taarifa ambazo gazeti hili limepewa na jirani wa staa huyo anayekimbiza na Wimbo wa Kiza Kinene akiwa amewashirikisha Sauti Sol kutoka Kenya, kwa sasa maisha yake yamekuwa supa kutokana na mjengo aliohamia.



“Nyie hamjui tu. Nandy amehamia huku Mbezi Beach ni jirani yangu kabisa lakini mjengo anaoishi si wa kitoto kuanzia kwenye geti, fensi hadi eneo kubwa la ndani ambalo unaweza kupaki hadi magari kumi ndani.

“Achilia ule aliokuwa akiishi Masaki (Dar) huu mjengo aliopanga ni zaidi aisee kwani hata kodi yake ipo juu, si chini ya milioni mbili kwa mwezi. Njooni tu muuone anavyoishi na matajiri wa huku tena hapa yeye anaishi na ndugu zake pamoja na wazazi wake,” alisema jirani huyo.



Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu walifunga safari hadi maeneo waliyoelekezwa na kukutana na mjumbe wa Mbezi Beach Makonde, Mtaa wa Makini.

“Hapa Nandy ni mtu ambaye hajikwezi siyo kama wasanii wengine, maana ana jina kubwa lakini pia anashirikiana nasi kwa kila kitu na hata akiwa na shida yake ya Kiserikali huwa anakuja. “Pia linapokuja suala la michango wa aina yoyote ile wanatoa maana mtaani kwetu huwa wananchi wanachangia michango mbalimbali ikiwemo ya ulinzi na usafishaji taka,” alisema mjumbe huyo.

Mjumbe huyo aliongeza kuwa, Nandy amekuwa ni mtu wa tofauti na mastaa wengine ambao huwa na tabia za kufungulia muziki sauti ya juu kiasi cha kuwakera majirani.



Baada ya kumalizana na mjumbe huyo, Risasi Jumamosi lilifika kwenye nyumba hiyo na kujionea namna ilivyo ya kishua lakini hata hivyo halikufanikiwa kuzungumza na Nandy kwa kuwa hakuwepo nchini.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini