RC Makonda awapa siku tano wakandarasi Watakaokaidi Kukiona | ZamotoHabari.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda, amewapa siku tano kuanzia jana Wakandarasi ambao miradi yao imekuwa ikisuasua kuhakikisha wanaanza kazi mara moja na kubainisha kuwa wakandarasi watakaokaidi agizo hilo Watakamatwa na Vyombo vya dola na mikataba yao kuvunjwa.

RC Makonda amesema wapo wakandarasi ambao Walidanganya kwenye nyaraka za kuomba tenda kuwa wana Vifaa vya kutosha, Wataalamu na Fedha za kutosha ili waatiwe kazi lakini baada ya kupata kazi wamekuwa wakikwama kufanya kazi kutokana na uhaba wa Vifaa, jambo linalopelekea miradi kutokamilika kwa wakati na kuleta Usumbufu kwa wananchi.


Miongoni mwa Miradi ambayo RC Makonda amesema imekuwa ikisuasua ni Ujenzi wa Mto Ng'ombe, Mfereji wa Buguruni Kisiwani, Tabata Roman Catholic, Barabara ya Kivule na Barabara ya Kawe.

Aidha RC Makonda amezionya Bodi za Manunuzi zitakazobainika kutoa tenda kwa wakandarasi kwa rushwa bila kuangalia uwezo wa Kampuni kuwa watachukuliwa hatua.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini