Mbwana Samatta arahisishiwa kazi kwa mabeki wa Liverpool | ZamotoHabari.


Mshambuliajiwa KRC Genk, Mbwana Samatta atakuwa katika wakati mzuri wa kuonesha uwezo wake mbele ya mabingwa watetezi wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, Liverpool baada ya safu yao ya ulinzi kupungua nguvu.

Mchezo huo wa tatu hatua ya makundi unatarajia kupigwa leo katika uwanja wa Luminius Arena mjini Genk, nchini Ubelgiji, ambako ndiyo maskani ya klabu hiyo anayokipiga nahodha wa Taifa Stars.

Taarifa zilizopo hii leo zinaeleza kuwa mlinzi machachari wa upande wa kulia wa Liverpool, Trent-Alexander Anold hajafanya mazoezi na klabu yake kutokana na kukumbwa na homa, hivyo hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Genk.

Genk ya Mbwana Samatta iko katika kundi E ikiwa na pointi moja katika nafasi ya mwisho baada ya kufungwa mechi moja na kutoka sare mechi moja. Napoli inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, huku Liverpool ikiwa na pointi 3 katika nafasi ya pili na Red Bull Salzburg ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 3.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini