Na woinde shizza Michuzi Tv, Arusha
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi ABDALLAH ULEGA Amewataka wafugaji na wafanya biashara wa mifugo kuunga mkono uuzaji ng’ombe kwa kilo na kuondokana na uuzaji mifugo kwa makisio, kwani litaleta thamani kwa mifugo pia maendeleo kwa mfugaji na tija kwa serikali kuweza kukusanya mapato yake
Akizungumza na wafugaji pamoja na wafanya biashara wakati akifunga mafunzo ya elimu kwa mfugaji na mfanya biashara juu ya uuzaji ng’ombe kwa kutumia mizani wilayani longido Mkoani Arusha Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah ulega amesema Minada yote nchi nzima lazima ng’ombe auzwe kwa kilo ili kuwe na kiwango maalumu cha uuzaji wa ng’ombe
ULEGA Amesema mfanya biashara yeyote atakaebainika kuhusika kununua au kuuza mifugo nje ya eneo lilotengwa kwa ajili ya uuzaji na ununuzi wa mifugo [MINADA] watachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwaita wahujumu uchumi
"mtu yeyote mfugaji ambaye atakutwa anauza Mifugo nje ya Mnada tutamchukulia hatua kali na siokulipa faini tu bali tutampeleka Mahakamani na tutamfungulia kesi ya uhujumu uchumi "alisema Ulega
ULEGA Akiwa katika moja ya viwanda vya kusindika maziwa kijulikanacho kwa jina la Kilimanjaro Freshi Amesema ameridhishwa na uendeshaji wa kiwanda hicho kwa kununua maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo na kuanzisha kitengo maalumu cha kutoa elimu kwa wafugaji jinsi gani ya kuweza kuwapa chakula bora ili waweze kutoa maziwa ya kutosha
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido Jumaa Muhina Aliwataka wafugaji hao kuachana na dhana yakufuga Mifugo mingi ambayo awanatija badala yake wafuge mifugo michache yenye tija
"nibora mfuge Mifugo mitatu au miwili yenye tija kuliko kufuga lundo la Mifugo ambayo aina faida yeyote, unakuta mtu anamifugo rundo na mungine ana mmoja lakini unakuta ukipima kwenye mizani unakuta uzito nisawa sasa sasahivi fugeni mifugo michache yenye tija "Alisema Muhina
Mmoja wa Mfugaji huyo aliyetambulika kwa jina la Olisienda Sadalla alishukuru kwa mafunzo aliyoyapata na kuhaidi kuwa watafuata sheria na kanuni zote zinazotakiwa na serikali ili wasiingie kwenye matatizo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji na wafanya biashara wa wilaya ya Longido (hawapo Pichani) wakati alipokuwa Kufuga mafunzo ya siku moja walikuwa wakifanya katika ukumbi wa St. Theresia uliopo Namanga mkoani Arusha, ambapo aliwataka wafugaji hao kutotorosha mifugo na kwenda kuuza nje ya nchi badala yake wafaate sheria na kanuni huku akibainisha kuwa atakae Kusuka hatua kali itachukuliwa dhidi yake ikiwepokufugwa(picha na woinde shizza, Arusha).
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah Ulega akionja maziwawyanatengenezwa na kamanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipotembelea Kiwanda hicho kuangalia namna kinavyofanya kazi(picha na Woinde shizza ,Arusha.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea kiwanda hicho jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha ambapo aliwasihi watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha na Woinde shizza, Arusha).
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments