David Moyes akabidhiwa tena mikoba ya West Ham | ZamotoHabari.



David Moyes ameteuliwa kuwa meneja mpya wa West Ham na atarejea kwa mara ya pili kwenye klabu hiyo. Mscotland huyo mwenye miaka 55 amesaini mkataba wa miezi 18 na ataanza na mechi ya nyumbani ya siku ya mwaka mpya dhidi ya Bournemouth.

Moyes anachukua mikoba ya Manuel Pellegrini, aliyetimuliwa baada ya kushindwa mechi ya Jumamosi 2-1 nyumbani dhidi ya Leicester wanaoonekana kubadilika sana.

Kocha huyo wa zamani wa Everton na Manchester United, aliyechukua mikoba kutoka kwa Slaven Bilic miaka miwili iliyopita, aliondoka mwishoni mwa msimu, baada ya klabu hiyo kuamua kuelekea upande mwingine na meneja wa zamani wa Manchester City Pellegrini.

Lakini Mchile huyo aliyeiongoza Hammers na kuwa nafasi ya kumi msimu uliopita, ametimuliwa kufuatia kushindwa mara nne mfululizo nyumbani juzi Jumamosi. Stuart Pearce na Alan Irvine, waliokuwa wasaidizi wa Moyes hapo nyuma, wanaweza kuwa tena wasaidizi wa kocha huyo.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini