Watu sita wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya lori na basi dogo la abiria kugongana jana Jumapili, majira ya saa 4 usiku jijini Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba chanzo chake ni dereva wa lori baada ya kuona korongo kubwa katikati ya barabara, akajaribu kulikwepa.
“Lakini wakati anahama kukwepa korongo hilo, tayari lile basi dogo la abiria lilikuwa limeshafika karibu, na bodi la lori likaliangukia basi hilo la abiria na kusababisha vifo na majeruhi. Tunaendelea kumsaka dereva wa lori kwani alikimbia usiku ule baada ya tukio hilo,” amesema Muroto.
Endelea kufuatilia taarifa hizi kwenye mitandao yetu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments