Polisi Yawashikilia, Kuwahoji Wasaidizi wa John Mnyika | ZamotoHabari.


Mwanza. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza liliwashikilia na kuwahoji wasaidiza wawili wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amewataja walioshikiliwa, kuwekwa mahabusu na kuachiwa baada ya mahojiano kuwa ni Ofisa Habari wa Chadema na Msaidizi binafsi wa Mnyika, Abdulkarim Muro pamoja na dereva wa Katibu Mkuu huyo, Said Haidan.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Desemba 30, 2019, Kamanda Muliro amesema watu hao walikamatwa kwenye nyumba moja iliyo karibu na hoteli ya Paradise eneo la Mahina jijini Mwanza baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo kwa watu wanaotiliwa mashaka kuwa ni wahalifu.

Mwananchi
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini