Wapiganaji wanne wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia wameuawa kwenye mashambulizi ya anga yaliyofanywa na majeshi ya Marekani katika maeneo mawili kwenye miji ya Qunyo na Caliyoow.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Marekani mashambulizi hayo yalifanyika siku moja baada ya takriban watu 90 kuuawa katika shambulizi la bomu lililotegwa ndani ya lori kwenye kituo cha ukaguzi chenye pilika pilika nyingi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Marekani hufanya mashambulizi ya anga mara kwa mara nchini Somalia katika juhudi za kuisaidia serikali dhaifu, inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyo katika mji mkuu wa Mogadishu na ambayo imekuwa ikipigana na kundi la Al-Shabaab kwa miaka kadhaa sasa.
Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika, AFRICOM imesema serikali za Marekani na Somalia zitaendeleza mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi kwa lengo la kuyadhoofisha.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments