Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amesema ameagiza kutafutiwa eneo kwa Mkali wa Muziki wa Bongofleva Tanzania Alikiba kufuatia kuwa mzaliwa wa Mkoa huo.
Mkuu wa Wiaya ya iringa Mjini Richard Kasesela akiwa na Alikiba kwenye Hafla kukabidhi vifaa maalum kwenye Hospitali ya Rufaa ya Iringa.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa maalum kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Richard Kasesela amesema Serikali itaendelea kushirikaina a na Alikiba kwa kuwa ameamua kurejesha anachokipata kwenye Mkoa aliozaliwa.
"Amekula Mbwa muangalieni tu, nimemwambia lazima awe na makazi hapa Iringa nimeagiza atafutiwe Kiwanja, na ajenge akija asifikie hotelini, akisimama Mkwawa pembeni asimame yeye King Kiba" amesema Kasesela
Kwa upande wake Alikiba Mwenyewe amesema lazima atatafuta nyumba ya kuishi kwenye Mkoa huo.
"Nafurahi kuwepo hapa Iringa, Baba yangu ni mzawa wa hapa Kijiji cha Chakalenga na huwa nakuja mara nyingi sana, sema sitangazi kwa sababu nahofia nisije nikashindwa kufanya nililolitaka" amesema Alikiba
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments