Mvua kubwa kunyesha mfululizo, Mikoa zaidi ya 10 yapewa tahadhari | ZamotoHabari.



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wakazi wa mikoa 13 nchini humo kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa inayotarajia kunyesha.

Taarifa ya TMA iliyotolewa jana imeitaja mikoa hiyo ambayo mvua hizo zinatarajia kunyesha kesho Jumamosi ni; Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Zanzibar.

TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni uharibifu wa miundombinu na mali kwa baadhi ya maeneo.

“Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, hatari kwa maisha ya watu kutokana na maji yanayotiririka kwa kasi au maji yenye kina kirefu, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” imeeleza taarifa hiyo

Taarifa hiyo inaeleza, Jumapili ya Desemba 22, 2019 kutakuwa na mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe Ruvuma, Singida, Dodoma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Jumatatu ya Desemba 23, 2019 mvua inatarajia kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Ruvuma.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini