Afariki Akizungumza naSimu Kwenye Chaji | ZamotoHabari.


Vumilia Kitang’enyi (19), mkazi wa Serengeti amekufa wakati akizungumza na simu aliyokuwa ameichomeka kwenye chaji, Jumatano Februari 5, 2020.

Taarifa zinadai kuwa, Vumilia alikutwa amekufa akiwa amepiga magoti huku ameshika simu mkono wa kushoto. Amekutwa na majeraha ya kuungua katika shavu la kushoto.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba amethibitisha kifo cha Vumilia lakini hakuwa tayari kueleza suala hilo kwa kina.

Mwenyekiti wa mtaa wa Sedeko eneo la Mugumu Mjini, Charles Chacha amesema Samwel Joseph maarufu Wazo alimkuta Vumilia ambaye ni mkewe akiwa amepiga magoti huku mkononi akiwa ameshika simu.

Amesema simu hiyo ilikuwa katika chaji na alipomchunguza alibaini amebabuka katika shavu lake la kushoto.


“Soketi aliyochomeka chaji inaonekana ilikuwa mbovu, naye kwa kuwa alikuwa anafua alikuwa na majimaji na katika sakafu kulikuwa na unyevunyevu kutokana na mvua zinazonyesha, inawezekana ni chanzo cha kifo chake,” amesema Chacha


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini