LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyojivunia ndani ya Yanga ni kuwa na aina ya wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na Haruna Niyonzima na Mapinduzi Balama.
Akizungumza na Spoti Xtra, Luc alisema kuwa amemtazama Niyonzima kwenye mechi zake zote alizoanza sio mwepesi wa kupoteza mipira anayopewa pamoja na uwezo wake wa kutuliza wachezaji wakiwa wamekasirika.
“Mchezaji mzuri unamtambua siku utakayomuona uwanjani kwa namna anavyofanya kazi yake kwa juhudi bila kuchoka na kuwa msaada kwa wengine na sio mzigo, ndivyo ilivyo kwa Niyonzima.
“Jaribu kumtazama kabla hajapewa mpira anatoa maelekezo, akiwa na mpira anatoa maelekezo kupitia viungo vyake, ni aina ya wachezaji ambao wanatakiwa kwenye timu inayotafuta ushindi, hawatofautiani na (Balama) Mapinduzi ambaye anajipa kazi ile aliyotumwa ndani ya uwanja,” alisema Luc.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments