Idadi ya waliokufa kwa Corona yafikia 722 China | ZamotoHabari.

Mpendwa Msomaji, tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi ZAMOTOHABARI APP.  Sasa ipo Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.

Idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya mripuko wa virusi vya corona imeongezeka na kufikia watu 722, ikipindukia rekodi ya vifo vilivyotokana na mripuko mwingine wa virusi vinavyofanana na hivyo vya SARS ambavyo viliikumba China Bara na Hong Kong miongo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa kamisheni ya afya ya taifa idadi nyingine ya watu 86 imepoteza maisha ambapo watano miongoni mwa hao wanatokea katika jimbo la Hubei, ambalo mripuko huko ulizuka Desemba. Kwa rekodi za kila siku kamisheni hiyo pia imesema visa 3,399 vimeripotiwa. 

Kwa hivi sasa zaidi ya watu 34,546 wameambukizwa virusi vyacoronakwa nchi nzima. Katika kipindi cha mwaka 2002 na 2003, ugonjwa wenye kufanana na huu unaosababaishwa na corona uliopewa jina la SARS ulisababisha vifo vya watu 650.

Meli ya starehe ya Japan Princess Diamond imekuwa ikiangaziwa zaidi katika kipindi hiki ambapo pia imeripotiwa visa vitatu vipya na kufanya jumla ya abiria wake 64 kuwekwa katika uangalizi maalumu kwa siku 14. Meli hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 3,700. Ijumaa Rais Xi Jinping wa China alizungumza na Rais Donald Trump na kuitaka Marekani kushiriki haraka katika kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona, na hasa kutokana na malalamiko ya baadhi ya nchi kuwazuia wasafiri kutoka China.

-DW



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini