Kwa Habari
za Uhakika na Haraka pakua APP yetu. ZAMOTOHABARI: Sasa
unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP mpya. Ukitaka kudownload kupitia
Playstore tafadhali BOFYA HAPA.
DUNIA ina mambo! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na yanayoendelea kwenye familia ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi ambapo kwa sasa kampeni ya kumng’oa mzazi mwenza na msanii huyo, Tanasha Donna inazidi kushika kasimakini kilicho karibu na familia hiyo kilieleza kuwa ndani ya familia hiyo kuna kampeni ya chini kwa chini ya kumng’oa Tanasha kwa Diamond kwani mama mkwe, Sanura Kassim ‘Sandra’ na wifi yake, Esma Khan hawamtaki kabisa.
“Kutokana na hilo ndiyo maana hata Tanasha alipoachia wimbo wake hivi karibuni, mama Diamond hakumsapoti kwa kuposti kama wengine walivyofanya pia hata kwenye uzinduzi wa EP yake Kenya hakuwepo wala ndugu wa Diamond yeyote.
“Hata ile ishu ya Diamond kufika Kenya kwa ajili ya kumsapoti Tanasha kwenye uzinduzi huo na kusema amepata dharura na kurudi Dar na meneja wake, ulikuwa ni mpango maalum kwa ajili ya kutekeleza kampeni yake,” kilieleza chanzo.
ESMA AONESHA WAZI
Katika kuonesha kweli kuna kampeni inaendelea juu ya Tanasha, dada wa Diamond, Esma alionesha wazi baada ya hivi karibuni akiwa beneti na mzazi mwenza na Diamond, Hamisa Mobeto ambaye awali wao kama familia waliwahi kumtolea maneno mabaya hadharani kwa kusema kuwa ni mshirikina kwani alikwenda kwa mganga ili kumloga Diamond amrudie.
Kwa Habari za Uhakika na Haraka pakua APP yetu. ZAMOTOHABARI: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP mpya. Ukitaka kudownload kupitia Playstore tafadhali BOFYA HAPA.Esma na Hamisa walionekana kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wamevaa nguo zinazofanana tena siku hiyohiyo ambayo kulikuwa na shughuli ya uzinduzi wa EP ya Tanasha huko Kenya.
Wajuzi wa mambo waliunganisha matukio na kudai kwamba Mobeto alikuwa nyumbani kwa kina Diamond na ndiyo maana hata mwanamuziki huyo alirudi na kuacha kuhudhuria kwenye uzinduzi, akidai kuwa amepata dharura.
Pamoja na picha hiyo, pia video ilisambaa mitandaoni ikimuonyesha Mobeto akiwa dukani kwa Esma, jambo ambalo linaonyesha kuwa wawili hao wameshibana vilivyo kwa sasa. Risasi Mchanganyiko liliwatafuta mama Diamond na Esma kwa njia ya simu ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo lakini hawakupatikana kwani simu zao ziliita kwa muda mrefu bila kupokelewa
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments