MBEYA: Watu Wasiojulikana Wamcharanga Kiongozi Huyu wa CHADEMA | ZamotoHabari.



Diwani wa Kata ya Isesye, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Mbeya Ibrahim Mwampwani, amecharangwa mapanga usoni na kichwani na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Februari 6, 2020, majira ya saa 4:00 usiku.

Kwa Habari za Uhakika na Haraka pakua APP yetu. ZAMOTOHABARI: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP mpya. Ukitaka kudownload kupitia Playstore tafadhali BOFYA HAPA.
Kwa mujibu wa Eatv.tv Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema, amesema kuwa diwani huyo tayari amekwishatoa taarifa Polisi na kwamba baada ya tukio lile alipelekwa hospitali na sasa amesharuhusiwa na anaendelea vizuri.

“Ilikuwa jana usiku wakati anatoka kwenye shughuli zake, akavamiwa na watu kama watano wakamjeruhi paji la uso na kichwani, ametibiwa na kesharuhusiwa na hawakumuibia chochote, tukio limetokea karibu na nyumbani kwake, yeye nimeongea naye analihusisha tukio hili na masuala ya kisiasa” amesema Mrema.

By Ally Juma.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini