Nyumba za Walimu Zageuka Danguro, Zasababisha Wanafunzi Kupata Ujauzito Shinyinga | ZamotoHabari.



Diwani wa Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga, Hassan Mwendapole amesema majengo ya nyumba za Walimu katika Shule ya Mwasele hivi sasa yamekuwa kama danguro, hali ambayo imepelekea Wanafunzi kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo

Mwendapole amesema, “Nyumba hizi za Walimu katika Shule ya Sekondari Mwasele zilijengwa tangu mwaka 2011 na sasa kuna mapagale tu, na yameshageuka kuwa kama guest house. Zinatumika kwa ngono na kusababisha kuwapo mimba za wanafunzi"
Kwa Habari za Uhakika na Haraka pakua APP yetu. APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP mpya. Ukitaka kudownload kupitia Playstore tafadhali BOFYA HAPA.
Inadaiwa kuwa, ujenzi wa majengo hayo ya nyumba mbili za Walimu bado haujakamilika, lakini yamekuwa yakitumika kufanya vitendo hivyo na baadhi ya Wanafunzi wamekamatwa wakifanya ngono

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini