Msanii wa filamu, Steve Nyerere amefunguka kuizungumzia post yake ya kutangaza kugombea Ubunge jimbo la Iringa mjini 2020. Mchekeshaji huyo amedai ana kila sifa ya kuweza kuiongoza Iringa kwa kuwa yeye ni kijana machachari.
“Mimi ni mwenyeji wa Iringa, nimezaliwa Iringa nimesoma Iringa, nimeona kwamba pale Iringa Mjini pana kila sababu ya kuwa kama Arusha, kama mwanza, nimeona mimi natosha kuwa Mbunge, hakuna kipengele kinachomkataza Mtu kutangaza nia , Mimi ni scania, Steve ni project kubwa Tanzania ”- Steve Nyerere
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments