Takriban watu 20 wamefariki baada ya kupigwa risasi kiholela na mwanajeshi mmoja wa Thai katika mji wa Nakhon Ratchasima, maafisa wa polisi wamesema.
Msemaji wa wizara ya ulinzi aliambia BBC Thai kwamba Jakraphanath Thomma, afisa wa madaraka ya chini alimshambulia mkuu wake kabla ya kuiba bunduki na risasi kutoka katika kambi ya kijeshi.
Baadaye aliwafyatulia risasi waumini waliokuwa katika hekalu na duka la jumla katika mji huo.
Polisi wameweka chapisho la mtu anayesakwaHaki miliki ya pichaAFP
Image caption Polisi wameweka chapisho la mtu anayesakwa
Picha zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii zimekuwa zikionyesha eneo ambalo ufyatuzi huo wa risasi ulifanyika karibu na duka la jumla.
Picha za vyombo vya habari zinaonekana zikionyesha mshukiwa huyo akitoka katika gari moja katika eneo moja la duka hilo la jumla katika wilya ya Muang na kuwafyatulia watu risasi kiholela.
Picha nyengine zilionyesha moto nje ya jengo hilo , huku kukiwa na ripoti kwamba ulisababishwa na gesi iliolipuka baada ya kupigwa risasi .
Moto katika jumla la jumla ulidaiwa kusababishwa na gesi ilipopigwa risasiHaki miliki ya pichaAFP
Image caption Moto katika jumla la jumla ulidaiwa kusababishwa na gesi ilipopigwa risasi
“Mwanajeshi huyo alitumia bunduki ya rashasha kuwapiga risasi watu wasio na hatia na kuwajeruhi wengi huku wengine wakifariki”, msemaji wa serikali Krissana Pattanacharoen aliambia chombo cha habari cha Ufaransa.
Msemaji wa idara ya ulinzi Luteni jenerali Kongcheep Tantravanich alisema kwamba watu 20 waliuawa.
Moja ya machapisho yake ya mitandao yanaonyesha picha ya selfie yake huku moto ukiwaka nyuma yake.
Hali ikoje hivi sasa?
Mamlaka imekizunguka kituo hicho huku ikijaribu kumtafuta mshukiwa ambaye anasemekana kuwa ndani ya jumba hilo.
Ramani ya eneo la shambulio hilo
Polisi imewaonya raia kusalia majumbani mwao.. gazeti la Bangkok post limeripoti kwamba mshukiwa huyo ambaye limesema ana umri wa miaka 32 amejificha ndani ya jumba hilo , lakini hilo halijathibitishwa .
Sauti zaidi za risasi zimesikika ndani ya jumba hilo.
Ni nini haswabacho mshukiwa huyo alichapisha katika mtandao wa kijamii?
Hatahivyo alituma chapisho jingine katika mtandao wake akiuliza iwapo ajisalimishe.
Lengo la mshukiwa huyo halijulikani.
Awali alikuwa amechapisha picha ya bunduki ndogo aina ya pistol na risasi tatu, pamoja na maneno ”ni wakati wa kujifurahisha” na hakuna mtu anayeweza kuzuia kifo”.
Ukurasa wake wa facebook sasa umeondolewa.
Gazeti la Bangkok Post limesema kwamba kamanda aliyeshambuliwa hadi kufa na mshukiwa huyo kanali Anantharot Krasae na kwamba mwanamke mwenye umri wa miaka 63 na mwanajeshi mwengine waliuawa katika kambi hiyo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments