Aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba Patrick Aussems, amesema kuwa amekuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki wa Simba wakimtaka arejee kuifundisha klabu hiyo.
Patrick Aussems
Kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii Aussems ameeleza kuwa anaiheshimu Simba na mashabiki wake wote lakini anawatakia kila la kheri na huenda watakutana tena siku nyingine.
‘Simba ni klabu kubwa, ina wachezaji wakubwa na mashabiki wa aina yake, nawatakia heri na siku moja pengine tutakutana tena’, ameandika.
Aussems alitimuliwa na Simba mwishoni mwa mwaka 2019 na nafasi yake kuchukuliwa na raia mwenzake wa Ubelgiji Sven Vandenbroeck.
Patrick Aussems @PatrickAussems
I am extremely touched by the thousands of messages received in the past few days asking me to come back. Simba SC is a big team with great players and wonderful fans ! I wish you the best and I am sure that one day we will meet again …
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments