Wabunge wametaka Serikali kuacha tabia ya kushikilia miili ya wanaofariki na ndugu zao kushindwa kulipa gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaofariki badala yake iwasamehe
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mussa Mbarouk wa Tanga wameyasema hayo wakati wakichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
Sugu amesema Serikali imekuwa ikisema hakuna Mtanzania anayekosa matibabu lakini wanashikilia maiti hospitalini na hatua hii inawanyima Watanzania kwenda kufanya ibada kwa ndugu zao wanaofariki kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu
Kwa Habari za Uhakika na Haraka pakua APP yetu. ZAMOTOHABARI: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP mpya. Ukitaka kudownload kupitia Playstore tafadhali BOFYA HAPA.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amejibu hoja hiyo kwa kusema Wananchi wanaokosa fedha za kulipia matitabu wanapaswa kwenda kwenye Dawati la Ustawi wa Jamii linalokuwepo katika kila Hospitali
Aidha, ameongeza kuwa hawana maiti ambayo wanaishikilia kwasababu ya madai ya gharama za matibabu kutokana na kuwepo kwa Dawati hilo
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments