Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema ni muhimu kuzingatia ushauri wa wataalamu na viongozi katika ugonjwa wa virusi vya Corona.
Kadhalika, amesema Corona haipaswi kupuuzwa kwani itasababisha watu kuumwa na wengine kufa.
“Pamoja na tahadhari zote tunazozichukua tatu ni za muhimu mno na zinaimbwa kote duniani,” aliandika Membe.
Membe aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kuwa “Tunawe mikono, tuepuke mikusanyiko na tukae majumbani mwetu,”.
Bernard Membe
Alisema kinachotakiwa ni kutekeleza maelekezo hayo na kuzingatia ushauri wa wataalamu na viongozi ” Tukipuuza tutaumwa na wengine tutakufa tusipuuze,”.
CORONA: Pamoja na tahadhari zote tunazozichukua, tatu ni za muhimu mno na zinaimbwa kote Duniani; Tunawe mikono, Tuepuke mikusanyiko na Tukae majumbani mwetu! Tutekekeze hayo na tuzingatie ushauri wa Wataalam na Viongozi wetu. Tukipuuza tutaumwa na wengine tutakufa! Tusipuuze!— Bernard K. Membe (@BenMembe) March 27, 2020
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments