Breaking News: Kocha wa Arsenal na Mchezaji wa Chelsea Wapata Maambukizi ya Corona | ZamotoHabari.



Klabu ya Arsenal imesema kuwa imefunga kwa muda kituo chake cha Mazoezi baada ya Kocha wao, Mikel Arteta kupata maambukizi ya virusi vya corona jana usiku

Kocha huyo kwa sasa amewekwa Karantini huku taratibu zote za Kiserikali katika kushighulikia suala hilo zikifuatwa. Klabu imesema inashughulikia pia kuwapima wengine wote waliokuwa karibu na Arteta kwa siku za karibuni

Aidha, Chelsea imesema imefunga kwa muda jengo la mazoezi la timu ya Wanaume baada ya Mchezaji wake, Callum Hudson-Odoi kugundulika kuwa na Maambukizi ya virusi vya Corona jana usiku

Chelsea imebainisha kuwa watu wote waliokuwa karibu na Hudson-Odoi kwa siku za karibuni katika timu ya Wanaume watatengwa kwa kufuata taratibu za Serikali. Watu hao ni pamoja na Wachezaji wenzake na Wafanyakazi

Klabu zote zimesema kuwa watu wote ambao hawakuwa karibu na Waathirika hao watarudi kufanya kazi katika siku za usoni


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini