Mchezo Kati ya Man City na Real Madrid Wahairishwa Kisa Mchezaji Kupata Corona | ZamotoHabari.



Mchezo wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Manchester City na Real Madrid wa hatua ya 16 Bora, uliokuwa uchezwe wiki ijayo, Jumanne Machi 17, 2020, umeahirishwa

Taarifa kutoka Man. City inasema “Uamuzi wa kuahirisha mchezo huo umefanyika kwa ushirikiano wa UEFA na kufuatia uthibitisho kuwa Wachezaji wa Madrid watakaa Karantini kwa siku 15, baada ya mchezaji kutoka timu ya mpira wa Kikapu ya Madrid kuthibitika kuwa na corona”

Aidha, imeeleza kuwa taarifa zaidi kuhusu tarehe mpya na masuala yote yanayohusu tiketi za mchezo huo uliokuwa ufanyike nyumbani kwa Man. City, katika uwanja wa Etihad, vitatolewa baadaye


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini