Coronavirus: Trump azuia safari za kutoka Ulaya kuingia nchini Marekani | ZamotoHabari.


Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuweka zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano, amesema safari zote za kutoka Ulaya zitazuiwa kwa siku 30 zijazo.

Lakini amesema ''hatua kali lakini zilizo na umuhimu'' hazitaihusisha Uingereza, ambayo ina visa 460 vya virusi vilivyothibitishwa.

Kuna visa 1,135 vilivyothibitishwa nchini Marekani na watu 38 wameripotiwa kupoteza maisha.

''Kuzuia visa vipya kuingia Marekani, tutaahirisha safari zote kutoka Ulaya,'' Trump alieleza.

''Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia usiku wa siku ya Ijumaa''. Aliongeza.

Tump amesema Umoja wa Ulaya ''umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari kama hizo'' zilizoanzishwa na Marekani.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini