Merkel akataa kufunga mipaka ya Ujerumani kujikinga na corona | ZamotoHabari.


Huku mripuko wa kirusi cha corona ukizidi kuyakumba maeneo mbalimbali duniani, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameweka bayana kwamba nchi yake haikusudii kufunga mipaka yake, akihoji kwamba ni jambo la maana zaidi kwa watu wanaowasili kutoka mataifa yaliyoathiriwa na kirusi hicho kujiwekea karantini wenyewe majumbani mwao.
 
Akizungumza kwenye mkutano wa dharura na waandishi wa habari mchana wa leo mjini Berlin, Merkel amesema ni muhimu kwa viongozi wa Ulaya kujadiliana njia nzuri na zenye ufanisi na zile ambazo hazina. Hata hivyo, kansela huyo amekiri kwamba wataalamu wanasema takribani asilimia 70 ya wakaazi wa Ujerumani wana uwezekano wa kuambukizwa kirusi hicho.Kufikia leo, 
 
Ujerumani imeripotiwa kuwa na watu 1,300 walioambukizwa, na watatu waliopoteza maisha, ikiwa ni idadi ndogo kabisa ikilinganishwa na maeneo mengine.Ujerumani haipakani moja kwa moja na Italia, ambayo ni kitovu cha maambukizi ya corona kwa Ulaya, ikiwa hadi sasa ina wagonjwa zaidi ya 10,000 na vifo zaidi ya 430. 
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini