Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Faustine Ndugulile, amesema sawa ya Chloroquine inapunguza ukali wa homa ya mapafu (Pneumonia).
Ndugulile ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter wakati akitoa elimu ya virusi vya Corona.
“Pia kufupisha muda wa kuugua homa hiyo kwa wagonjwa wa Corona,” aliandika Dk Ndugulile.
Amesema kuwa dawa hiyo haiponyi bali inapunguza makali ya ugonjwa, hivyo wananchi waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona.
Elimu ya Corona: Dawa ya Chloroquine inapunguza ukali wa homa ya mapafu (pneumonia) na pia kufupisha muda wa kuugua homa hiyo kwa wagonjwa wa Corona. Hivyo dawa hii haiponyi bali inapunguza makali ya ugonjwa.— Faustine Ndugulile (@DocFaustine) March 20, 2020
Tuendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona.#covid19Tanzania
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments