Filamu ya Contagion ya Miaka 10 iliyopita yatabiri Kutokea Mlipuko wa Virus | ZamotoHabari.


Filamu ya Contagion ya miaka 10 iliyopita yatabiri kutokea mlipuko wa Virus

vya Corona ?, wapenzi wa ‘movies’ waisaka.

Mwaka 2011 ilitoka filamu ya Contagion nchini Marekani na haikupata bahati ya kujizoelea umaarufu mkubwa kama zilivyo ‘movie’ nyingine.

Licha ya kuwahusisha wachezaji maarufu wakiwemo, Matt Damon, Jude Law, Gwyneth Paltrow, Kate Winslet na Michael Douglas, filamu hiyo ilishika nafasi ya 61 miongoni mwa filamu zilizoingiza mapato makubwa kwa mwaka huo.

Lakini filamu ya Contagion imerejea ghafla kwenye orodha ya filamu zilizopakuliwa zaidi kwenye Apple’s iTunes Store nchini Marekani, huku jina lake likisakwa zaidi katika Google.

Warner Bros. – studio ambayo ilitengeneza filamu ya Contagion – imesema kuwa ilikuwa ni ya 270 kwenye filamu maarufu mwezi Disemba, wakati taarifa ya kwanza ya mlipuko wa Virusi vya Corona au Covid-19 ilipotangazwa nchini Uchina .

Miezi mitatu baadae , Contagion iko nyuma ya filamu nane za Harry Potter franchise.

Yote hayo yamesababishwa na virusi vya corona na kufananishwa kwa mlipuko wa hivi karibuni wa virusi vya corona na kilichoongelewa katika filamu miaka 10 iliyopita.

Sanaa ya maigizo ya maisha Life imitating artMatt Damon an Gwyneth Paltrow pose for pictures during the Contagion premiere in 2011

Gwyneth Paltrow alikua akicheza kama mgonjwa wa mlipuko katika filamu Contagion
Vyombo kadhaa vya habari vimeanza kuandika habari ya filamu hii ya Contagion namna inavyozidi kujizoelea umaarufu na watu kuitafuta kupitia mitandaoni kutokana na kile kilichozungumza au guizwa kuendana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona.

Katika filamu hiyo, nafasi ya mfanyabiashara mwanamke (ilichezwa na Paltrow) ambaye anaonekana akiuliwa na ugonjwa wa ajabu wa virusi alivyovipata alipokua katika safari yake ya Uchina, lakini baada ya kusababisha dharura ya afya kote duniani.

Uhusiano na Uchina ni mojawapo ya mambo mengi ya maisha halisia ambayo yameongeza umaarufu wa filamu hii katika wiki za hivi karibuni, huku watazamaji wakiitazama sana filamu ya Contagion.

 .

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini